Falsafa ya jazanda ya uongozi na mauko katika methali za jamii ya Wanyore: Mtazamo wa kisemantiki

Authors

  • Henry F Andele Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Masinde Muliro, Kenya
  • Susan C Choge Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Masinde Muliro, Kenya
  • Fred S Wanjala Chuo Kikuu cha Kibabii, Kenya

DOI:

https://doi.org/10.51317/ecjkisw.v2i1.175

Keywords:

falsafa, jazanda, kisemantiki, mauko

Abstract

SWAHILI

Makala hii inatokana na utafiti ambao uliazimia kutathmini falsafa ya jazanda katika methali za Wanyore kwa mtazamo wa kisemantiki. Madhumuni ya makala yenyewe yanahusu falsafa ya uongozi na mauko katika methali za Wanyore. Nadharia ya Uhusiano ya Sperber na Wilson (1986) na iliyoendelezwa nao (2004) ndiyo iliyoongoza makala hii. Nadharia hii ilitumiwa kufafanulia maana za methali katika jamii ya Wanyore. Data ilikusanywa kutoka kwa Wanyore wanaoishi katika kaunti ndogo ya Emuhaya na Luanda katika kaunti ya Vihiga. Makala haya yalitumia njia za uchanganuzi matini na mahojiano kukusanya data. Vifaa vilivyotumiwa vilikuwa ratiba ya usaili na tepurekoda. Data ilichanganuliwa kimaelezo kwa kunukuu methali za Kinyore, kisha zikatafsiriwa na kufasiriwa katika Kiswahili hatimaye falsafa ya jazanda ya uongozi na mauko ikaainishwa na kuelezwa. Matokeo ya kazi hii yatachangia kueleweka kwa falsafa ya jazanda ya uongozi na mauko miongoni mwa wanajamii.  Pia, yatakuwa nyongeza ya marejeleo kwa watafiti katika uwanja wa methali.

Downloads

Download data is not yet available.

Downloads

Published

2020-12-15

Issue

Section

Articles

How to Cite

Falsafa ya jazanda ya uongozi na mauko katika methali za jamii ya Wanyore: Mtazamo wa kisemantiki. (2020). Editon Consortium Journal of Kiswahili, 2(1), 163-172. https://doi.org/10.51317/ecjkisw.v2i1.175